Barua kwa Mpenzi wangu Azimio

(0 User reviews)   2174   1184
By OLS Admin Posted on Mar 20, 2021
In Category - Special Publications
Prof. Issa Shivji 978-9976-9903-6-2 Kavazi la Mwalimu Nyerere 2018
Utungo huu wa Prof. Issa Shivji wa Barua kwa Mpenzi Wangu ni ungamo la mtu ambaye kwa sehemu kubwa ya maisha yake ameamini na kushiriki katika mapambano hayo ya kuwatetea wanyonge. Huyu ni mtu ambaye alilipokea na kulikubali Azimio kuwa ni chombo cha kuleta ukombozi, na katika utungo huu anatudhihirishia kuwa bado anaamini hivyo. Amekataa ‘kugeuka jiwe.’ Usaliti na ‘‘uritadi’’ wa wale waliopokea hatamu za kulitekeleza Azimio haujamkatisha tamaa.

Baada ya Uhuru, chama tawala cha Tanzania Bara cha Tanganyika African National Union (TANU) kilichoongozwa na Mwalimu J. K. Nyerere kilishtuka baada ya kuona jinsi nchi ilivyokuwa ikijenga mfumo wa kitabaka usiowajali wanyonge.

Mwaka 1964 palitokea jaribio la maasi ya wanajeshi. Nusura yafanikiwe. Mwaka 1966 wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam (CKKD), chuo kikuu pekee nchini Tanzania wakati huo, waliandamana kupinga sheria ya kuwalazimisha kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa kwa miaka miwili. Nyerere alishtuka, akawafukuza chuoni. Migomo na malalamiko ya wafanyakazi nayo yalikuwa yakiongezeka.

Mambo yote haya yaliungana kumshawishi Nyerere na Chama tawala cha TANU kwamba hali haikuwa shwari; kwamba ili kuepusha shari, kudumisha uzalendo na mshikamano, na kurejea kwenye malengo ya awali ya kupigania uhuru, ilibidi hatua za haraka zichukuliwe ili kubadili mwelekeo wa nchi. Hivyo mwishoni mwa mwezi Januari 1967 halmashauri ya TANU ilikutana Arusha na kupitisha Azimio la Arusha. Azimio hilo lilitangazwa rasmi tarehe 5 Februari 1967. Huu ndio muktadha wa kihistoria-kijamii wa utungo huu Barua kwa Mpenzi Azimio wa Issa Shivji.

Utungo wa Barua kwa Mpenzi Wangu ni ungamo la mtu ambaye kwa sehemu kubwa ya maisha yake ameamini na kushiriki katika mapambano hayo ya kuwatetea wanyonge. Huyu ni mtu ambaye alilipokea na kulikubali Azimio kuwa ni chombo cha kuleta ukombozi, na katika utungo huu anatudhihirishia kuwa bado anaamini hivyo. Amekataa ‘kugeuka jiwe.’ Usaliti na ‘‘uritadi’’ wa wale waliopokea hatamu za kulitekeleza Azimio haujamkatisha tamaa. Anaamini kuwa mradi maonevu na unyonyaji ungalipo duniani, mapambano ya wanyonge ya kujitoa katika hali hiyo na kutafuta usawa na haki hayawezi kukoma, na kwa sababu hiyo Azimio halijapitwa na wakati.

Mtunzi anasisitiza kuwa Azimio ni sura, historia, urathi, mali, chombo na matumaini ya wanyonge ambao daima wako tayari kulilinda, kulitetea na hata kulifia. Hivyo pamoja na maombolezo kuhusu ‘kifo’ cha Azimio, hatimaye utungo unamalizikia katika hali ya matumaini.

There are no reviews for this eBook.

0
0 out of 5 (0 User reviews )

Add a Review

Your Rating *

Related eBooks