Simulizi za Azimio la Arusha

(0 User reviews)   2191   1371
By OLS Admin Posted on Mar 23, 2021
In Category - Special Publications
Prof. Issa Shivji, Bashiru Ally 978-9976-9903-5-5 Kavazi la Mwalimu Nyerere 2017
Simulizi za Azimio la Arusha ni chapisho maalum la Kavazi la Mwalimu Nyerere liloandaliwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka hamsini ya kuzaliwa kwa Azimio. Simulizi hizi zinachambua, kwa muhtasari, mpangilio wa Azimio na misingi yake kwa mtazamo wa kifalsafa na kiitikadi na hotuba ya Mwalimu Nyerere aliyoitoa katika semina ya wakuu wa serikali.

Ni kawaida siku hizi kuwasikia baadhi ya wasomi, wanasiasa na wanahabari wakisema kwamba nchi yetu imekosa dira. Mara nyingi wanasema hivyo bila kuangalia kwa undani kuhusu dhana na maana ya dira. Sura ya Kwanza inachambua, kwa muhtasari, mpangilio wa Azimio na misingi yake kwa mtazamo wa kifalsafa na kiitikadi. Matumaini yetu ni kwamba uchambuzi huu utaongeza kiwango cha uelewa wa wasomaji kuhusu dhana na maana ya dira.  Sura ya Pili ni Azimio lenyewe.

Sura ya Tatu ni sehemu ya hotuba ya Mwalimu Nyerere aliyoitoa katika semina ya wakuu wa serikali, mashirika ya umma na wafanyabiashara mwaka 1989. Katika kipindi cha kwanza cha uongozi wa awamu ya pili, chini ya Mzee Mwinyi, vuguvugu la kupinga Azimio lilikuwa limeshaanza kwa hoja kwamba limepitwa na wakati. Wengi wa wasomi wetu walikubaliana na hoja hizo. Aidha, tulikuwa tumeanza kulegeza masharti ya biashara, na kukubali masharti ya taasisi za fedha za kimataifa pamoja na wafadhili. Mwalimu alitoa hotuba hiyo katika mazingira hayo na alitumia fursa hiyo kuwaonya viongozi na watawala wasifanye kosa la kuachana na Azimio kwa sababu ndilo hasa lililotoa matumaini kwa wanyonge.

Hata hivyo, watawala hawakumsikiliza. Katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama cha CCM, uliofanyika huko Zanzibar mwaka 1991 chini ya Mzee Mwinyi, viongozi wa juu wa chama walifanya maamuzi ya kulegeza masharti ya uongozi, yaani, kuruhusu viongozi wa chama na serikali kujilimbikizia mali. Sura ya Nne ni hotuba ya Mzee Mwinyi inayoelezea na kutetea maamuzi ya Zanzibar. Katika hotuba hiyo, Mzee Mwinyi anasisitiza kwamba maamuzi yale yalikuwa ni tafsiri mpya ya Azimio ili nchi iweze kuendana na wakati!

Sura ya Tano na ya mwisho ni uchambuzi wa Miongozo miwili ya Chama, Mwongozo wa 1971, na Mwongozo wa 1981.

Ni matumaini yetu kwamba maandishi haya yatavisaidia vizazi vya leo kuelewa kwa undani historia ya Azimio la Arusha na kutoa mchango wao katika kukomboa nchi na bara letu.

There are no reviews for this eBook.

0
0 out of 5 (0 User reviews )

Add a Review

Your Rating *

Related eBooks