Tukate Mirija ya Unyonyaji

(0 User reviews)   2523   1392
By OLS Admin Posted on Mar 23, 2021
In Category - Kutoka Kavazini
Julius K. Nyerere 978-9976-9903-6-2 Kavazi la Mwalimu Nyerere 2017
Hotuba hii ya Mwalimu, aliyoitoa nusu karne iliyopita, inatoa nafasi nyingine ya kutufikirisha na kutuongoza kila tutakapokuwa tunatafakari jinsi ya kuendeleza ukombozi wa wavujajasho kwa kutumia itikadi na nadharia ya kimapinduzi. Aidha, hotuba hii inatuelekeza jinsi ya kupanga mikakati ya kimapinduzi kwa sababu mapinduzi, hususan mapambano dhidi ya ubeberu na vibaraka wake, sio lelemama na hayaji kwa kulalama.

Mwalimu alizungumzia kwa mara ya kwanza kuhusu Ujamaa akiwa anafungua mkutano wa wakuu wa mikoa tarehe 22 Januari 1967. Hotuba aliyoitoa Mwalimu mbele ya Halmashauri Kuu, ambayo iliwekwa katika kumbukumbu za mkutano huo wa tarehe 26 Januari 1967, na ambayo tuliipata kutoka katika maktaba ya Mwalimu huko Butiama, ilikuwa sawa na ile aliyoitoa mbele ya mkutano wa wakuu wa mikoa.

Jambo la pili alilozungumzia Mwalimu ni kuhusu mtazamo wa kujitegemea. Mwalimu alisisitiza kwamba tukiendelea kutegemea misaada kutoka nje tutahatarisha uhuru wetu na hasa uwezo wetu wa kujiamulia mambo yetu wenyewe. Akifananisha misaada kutoka nchi za kibeberu na zaka zitolewazo kanisani kila Jumapili, Mwalimu alibainisha kwamba hakuna nchi iliyoendelea kwa “zaka za Jumapili” kwa sababu wanaotoa misaada ya shilingi moja wanachuma mamilioni ya hela kutokana na unyonyaji wa jasho la watu wetu na utajiri wa nchi.

Hotuba hii ya Mwalimu, aliyoitoa nusu karne iliyopita, inatoa nafasi nyingine ya kutufikirisha na kutuongoza kila tutakapokuwa tunatafakari jinsi ya kuendeleza ukombozi wa wavujajasho kwa kutumia itikadi na nadharia ya kimapinduzi. Aidha, hotuba hii inatuelekeza jinsi ya kupanga mikakati ya kimapinduzi kwa sababu mapinduzi, hususan mapambano dhidi ya ubeberu na vibaraka wake, sio lelemama na hayaji kwa kulalama.

Matumaini yetu ni kwamba usambazaji wa nyaraka tulizogundua katika utafiti wetu utasaidia kizazi hiki na vizazi vijavyo kujua na kuchambua historia ya nchi yao, hususan kupitia nyaraka mbalimbali za Mwalimu pamoja na zile zilizoandikwa na wengine juu yake. Tofauti na watafiti wengine, sio nia yetu kuhodhi nyaraka tulizogundua katika utafiti wetu kana kwamba ni mali yetu. Nia yetu hasa ni kuzihifadhi nyaraka hizi kwenye Kavazi la Mwalimu Nyerere na kuwawezesha wanazuoni na watafiti kuzisoma na kuzichambua ili waweze kujua na kuwajuza Waafrika historia halisi ya bara lao.

There are no reviews for this eBook.

0
0 out of 5 (0 User reviews )

Add a Review

Your Rating *

Related eBooks