Insha Tatu za Kifalsafa

(0 User reviews)   2213   1375
By OLS Admin Posted on Mar 23, 2021
In Category - Occasional Papers
Julius K. Nyerere 978-9976-9903-2-4 Kavazi la Mwalimu Nyerere 2019
Hazina kama hii ya mawazo, fikra na maandishi mahiri ya Mwalimu katika insha, yenye ladha ya kipekee ni nadra sana kupatikana kutoka kwa wanasiasa wa kisasa. Tuna imani kwamba mbali ya kufarijika, kizazi hiki na vizazi vijavyo vitakuwa warithi waaminifu, waadilifu na wabunifu wa lulu hii ya ufahamu na usomi.

Kitabu hiki kina insha tatu zilizoandikwa na Mwalimu kwa nyakati tofauti na inavyoelekea, kwa sababu mbalimbali. Kadri tunavyojua, makala haya hayajawahi kuchapishwa. Tuliyakuta katika maktaba yake ya Butiama yakiwa karatasi zilizochapwa kwa taipu. Tunayachapisha katika kitabu hiki katika uasilia wake, bila kuyahariri au kuyabadilisha maneno isipokuwa tu kusahihisha zile sehemu ambazo ni wazi zina makosa ya upigaji chapa, kwa mfano, uwekaji nafasi kati ya neno na neno. Ndio maana mara nyingine tunakuta maneno mengine hayapo, ama kwa sababu yalifutika au yalirukwa. Hata hivyo tumeridhika kwamba yanasomeka vizuri na mantiki na malengo yake yanaeleweka kwa ufasaha kabisa.

Tunafurahi kupita kiasi kuweka hadharani urathi huu wa Mwalimu. Hazina kama hii ya mawazo, fikra na maandishi mahiri yenye ladha ya kipekee ni nadra sana kupatikana kutoka kwa wanasiasa wa kisasa. Tuna imani kwamba mbali ya kufarijika, kizazi hiki na vizazi vijavyo vitakuwa warithi waaminifu, waadilifu na wabunifu wa lulu hii ya ufahamu na usomi.

Nawaachia wasomaji wenyewe wasome insha hizi na kuonja utamu wake, sio tu ujumbe uliyomo ambao ni wa msingi kabisa, lakini pia mitindo yake, msamiati uliyotumika na ladha yake. Ukiweza kufananisha na chakula, insha hizi ni chakula cha kulamba polepole sio cha kuvamia mara moja; kadri unavyoramba, ndivyo unatamani kisiishe ili uendelee kuramba.

There are no reviews for this eBook.

0
0 out of 5 (0 User reviews )

Add a Review

Your Rating *

Related eBooks